GET /api/v0.1/hansard/entries/840696/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 840696,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/840696/?format=api",
    "text_counter": 559,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": ", au training na pia kutengenezewa barabara. Uchafu pia unachomwa na hayo yamo katika Mswada huu. Bi. Spika wa Muda, tukisema tutapiga msasa Mswada huu, mambo mengi yameenda kwa ugatuzi. Hasa kwa kuwa madini haya yanapatikana katika kaunti, watu wameweza kupata cheche nyingi na kusema kuwa mambo mengi yamewekwa kwa Serikali kuu. Waziri ambaye yuko katika Serikali kuu atakuwa na mamlaka, na hii ndio sababu tunasema kwamba kutakuwa na wahuni wengi wanaoitwa cartels katika Serikali kuu. Wahuni hawa watanyonya haki na rasilimali ambazo zitapatikana katika sehemu ile ya chini; na hiyo ndiyo sababu watu wameenda kwa ugatuzi. Kwa hivyo, hayo mamlaka makubwa yaliyopewa waziri katika Serikali kuu yanatakikana yavunjwe, na watu wa Kenya waseme jinsi wanavyotaka ili mambo yaendelee vizuri. Bi Spika wa Muda, hatuwezi kusema kwamba Mswada huu utupiliwe mbali. Huu ni Mswada unaohitaji kupigwa msasa ili Wakenya waweze kusema ya kwamba hii ni sheria inayofaa. Lakini tukisema kwamba tutautupa Mswada huu, tutakuwa tumepoteza akili kubwa na jasho jingi ambalo Kamati hii walitumia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}