GET /api/v0.1/hansard/entries/840899/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 840899,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/840899/?format=api",
    "text_counter": 177,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kuzungumza. Tulipiga kura kama wenzangu walivyosema na tukakataa na tukafaulu na Mhe. Naibu Spika wa Muda akakubali. Lakini baadaye, kukawa kuna wengine ambao wanataka tupige kura kupitia tarakilishi. Kwa hivyo, tukaweka kadi zetu na zikaonyesha idadi kubwa zaidi ya mia tatu hamsini na mbili. Kukawa na utatanishi kwa sababu hiyo idadi si ya jumla ya Bunge kwa hivyo, haiwezekani. Makarani wakaanza kutuhesabu sisi na vidole kwa kweli, huwezi kuhesabu watu katika chumba kikubwa kama hiki kwa vidole. Kwa hivyo, hiyo kura haiwezi kuwa halali."
}