GET /api/v0.1/hansard/entries/842435/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 842435,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/842435/?format=api",
"text_counter": 53,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, hawa ni watu ambao tangu wafurushwe makwao, wamekuwa wakitazama kwa runinga kwa miaka wengine wakipata fidia katika maeneo mengine ya taifa letu. Hili ni jambo ambalo lazima liagaliwe kikamilifu. Hatutazungumza mambo ya IDPs milele katika taifa letu. Wale IDPs waliopata fidia ni wale waliokuwa kwenye mahema. Hata hivyo, tunajuwa kuwa katika jamii zingine ni vigumu sana kuwacha watu kwa hema. Watu walijiunga na wengine. Kwa lugha ya Kimombo wanaitwa integrated IDPs. Wengi wao ndio wako na hii shida na ni muhimu kuangalia jambo hili. Kuna wale ambao walifurushwa wakati wa ghasia baada ya uchaguzi wa 2007. Lakini pia kuna wale ambao, kama alivyosema Sen. (Rev.) Waqo, huathirika wakati kuna mikasa kama ya moto ambayo huendelea. Kwa mfano, jana kumekuwa na mkasa wa moto kule Mukuru na Hazina. Nimetoka Pumwani na idadi kubwa ya wananchi walikuja pale kwa sababu wengi wao mali yao imechomeka kule Matopeni, Majengo. Hawa wananchi wanahitaji kujenga makao yao. Wanahitaji misumari, blanketi, chakula na vitambulisho. Watoto wao hata hawana nguo za kwenda shule. Bw. Naibu Spika, ni jambo la kusikitisha kwa sababu, kama kiongozi, wananchi kama hao wanapokuja kwangu, siwezi kuwaaambia kuwa sina msaada. Ili niweze kuwasaidia ni lazima niingie mfukoni. Hata nikimaliza shughuli hapa ni lazima niende kuwasaidia. Mbunge katika Bunge la Taifa labda atatumia hazina ya National Government Constituency Development Fund (NG-CDF) kuona vile atawasaidia. Gavana ana kitita kikubwa sana ambacho ni mabilioni ya pesa, lakini sisi tunakosa uwezo wa kuwasaidia wananchi wakipata shida kama hizi. Shida hizi zote hutokana na mambo ya ardhi. Watu wengi wanafurushwa kwa sababu kuna mabwenyenye ambao wako na vyeti vya kumiliki ardhi. Wanataka kuwafurusha kwa kuteketeza ili waweze kuchukua makao hayo. Nimefurahi leo kwa sababu katika Gazeti Rasmi la Serikali, yaani Kenya Gazette, kuna Hati Miliki nyingi sana ambazo zimepigwa marufuku kwa sababu zilikuwa za ardhi ambayo wananchi wamenyang’anywa. Bw. Naibu Spika, nimgeomba Kamati ambayo itapata ombi hili kutuhusisha kwa sababu jambo hili linahusu watu wa Kibera. Najua kwamba wengi wameumia sana. Juzi wengine walifukuzwa pahali panaitwa Kwa DC kwa sababu ya ujenzi wa barabara na wakaachwa hivyo. Ni jambo la uchungu sana ukiona watoto wakikuangalia kwa matumaini; wamekosa imani na hawajui watafanya nini. Ningependa Kamati hiyo ituhusishe, na sisi kama viongozi, tukumbuke kuwa maisha ya Mkenya wa kawaida au mnyonge ni lazima iwe muhimu kwetu. Tusiwe tu tunaangalia maneno ambayo yanatuhusu kama viongozi na kusahau yale ambayo yana husu Wakenya wa kawaida au wanyonge. Tuna sahau yale ambayo yana wahusu Wakenya wa kawaida, walio wanyonge. Ingekuwa ni Wakenya wale mabwenyenye ama wale ambao wana uwezo katika makao ya Karen, Kileleshwa au Kilimani ambao hawana makao, ambao idadi kama hii imesemwa kwa Ombi hii, tungekuwa na shida kubwa sana. Lakini kwa sababu mara nyingi tunasema ni Mkenya mnyonge ambaye labda hana uhusiano na wewe, tuna wachana nao. Tukumbuke kila siku ya kwamba hawa ndio tunafaa kuwakilisha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}