GET /api/v0.1/hansard/entries/843061/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 843061,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/843061/?format=api",
"text_counter": 36,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii kuchangia Statement ya Sen. (Rev.) Waqo. Ni jambo la kusikitisha kwamba baada ya miaka 57 tangu Kenya ipate Uhuru, bado kuna mauaji ya kiholela ambayo polisi wameshindwa kukomesha. Mauaji kama hayo yanaendelea na la kusikitisha ni kwamba wasio na hatia kama hayati Sharon na wengine wanakumbana na vifo katika hali za kutatanisha lakini Serikali na polisi wameshindwa kutatua. Hiyo si mara ya kwanza mauaji ya kiholela kufanyika kwa sababu tumeshuhudia mauaji mengi katika nchi ya Kenya. Juzi, mwanamume mmoja kule Kayole alidaiwa kusukumwa na kuanguka lakini kifo chake bado hakijachunguzwa. Jukumu la kwanza la Serikali ni kutetea maisha na mali ya wananchi wake na wale wanaoishi katika nchi ya Kenya. Ikiwa Serikali imeshindwa kufanya jambo hilo---"
}