GET /api/v0.1/hansard/entries/844539/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 844539,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/844539/?format=api",
"text_counter": 456,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": " Ahsante Bwana Spika. Nimesimama kuiunga mkono Ripoti hii. Bado napinga wazo la kumtoa huyu dada yetu, Ashubwe. Sababu moja ambayo napinga ni kuwa wanadamu kadri tunavyoishi huko nje tuna maadui wengi sana. Hakuna yule ambaye hakutakii mazuri atakaye kuunga mkono. Kwa hivyo, katika wale watu wa Central Organisation of Trade Unions (COTU) ambao walipinga uchaguzi wa huyu mama, pengine wengine ni watu walikosana naye kwa njia moja ama nyingine. Kwa hivyo, mimi sioni kama hiyo ni sababu ambayo inapaswa ichukuliwe kwa uzito kumnyima mama huyu nafasi. Naomba marekebisho yafanyike na mama huyu achukuliwe kuwa mmoja wa Tume hii. Naunga mkono Ripoti hii hasa kwa upande wa Dkt. Amani Yuda Komora. Ni mtu ambaye namjua kwa undani sana na ambaye amefanya kazi sehemu nyingi. Namjua kwa njia zote. Ako na uzoefu wa kazi."
}