GET /api/v0.1/hansard/entries/846923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 846923,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/846923/?format=api",
"text_counter": 78,
"type": "speech",
"speaker_name": "Rabai, ODM",
"speaker_title": "Hon. William Mwamkale",
"speaker": {
"id": 2672,
"legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
"slug": "william-kamoti-mwamkale"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kabisa, namshukuru Mhe. Owen aliyeleta Hoja hii. Ni Hoja ambayo kweli wakati wake umefika. Nataka niambie Nyumba hii ya kwamba jimbo la Pwani ndilo jimbo ambalo kwa sasa tunaweza kusema halina mmea ambao umeorodheshwa kama mmea wa kuboresha uchumi wa nchi hii. Kwa Kimombo wanasema cash crop . Hakuna. Hiyo inasikitisha sana. Imefanya mpaka ukulima umedorora kwa sababu si mkorosho wala mnazi. Hii ni mmea ambayo wakulima wanapozingatia kilimo chake, hawaoni faida. Hakuna soko ambalo Serikali inagharamia. Hoja hii kwa ufupi inasema kwamba kiangazi kinapouma nchi hii, basi kule Pwani ambako wanategemea sana mnazi, hasa Rabai ambapo mnazi umekithiri, mnazi huwa unakatika vilele. Na mnazi unapokatika, huo ndio mwisho wake. Mnazi unapokatika, yule mkulima aangaliwe kwa sababu mnazi unachukua miaka 15 kulelewa mpaka uanze kuzaa nazi. Mahali mnazi unapandwa, hakuna mti ama mmea mwingine unaweza kufanya vizuri. Kwa hivyo, huwa ni tegemeo la yule mkulima. Matarajio ya mkulima ni kwamba baada ya hiyo miaka kutimia, ataanza kuvuna na aendelee kuvuna. Lakini kwa bahati mbaya, kiangazi kinapoingia na mti huu kukatika, mkulima hupata hasara kubwa. Tuko katika nchi moja. Inafaa Serikali, kupitia Wizara ya Kilimo, iangalie kule ambako kiangazi kilikithiri iwafidie waathiriwa. Tumeshaona ng’ombe wanapofariki wakati wa kiangazi, Wizara ikiwajibka na kuchukua orodha ya watu waliopoteza ng’ombe wao kwa kiangazi na kuwafidia. Fidia hiyo pia tunaiona wakati mkahawa unapoathirika. Serikali huingilia. Lakini mti wa mnazi unapoathirikwa na kiangazi na kukatika, Serikali haishughuliki. Ukweli ni kwamba mkulima huwa amepata hasara. Huu ni mti ambao umemchukua mkulima zaidi ya miaka 10 kuulea. Hakuna vile anaweza kupanda mti mwingine ufanye vizuri baada ya miaka michache. Kwa hivyo, mkulima wa mnazi anastahili kupewa fidia kama vile wakulima wengine wanavyoangaliwa kiangazi kinapowaathiri."
}