GET /api/v0.1/hansard/entries/846930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 846930,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/846930/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ganze, ODM",
"speaker_title": "Hon. Teddy Mwambire",
"speaker": {
"id": 13334,
"legal_name": "Teddy Ngumbao Mwambire",
"slug": "teddy-ngumbao-mwambire-2"
},
"content": "Mimi siongei tu kwa sababu natoka Pwani, ama kwa sababau ninawakilisha wakulima. Mimi ni mmoja wa wakulima na watumizi wa bidhaa zinazotoka kwa mnazi. Mimi ni mshirikishi mkuu ambaye niko hapa kwa hisani ya mnazi. Kumbukumbu zinasema kwamba kabla Kenya ipate Uhuru, mnazi ndio mmea ambao ulikuwa unashamiri zaidi kule Pwani. Ulikua mmea uliosisimua uchumi. Lakini kukawa na matatizo baada ya Kenya kupata Uhuru. Mimea yote iliyokuwa imepewa umuhimu wa kiuchumi kule Pwani, ukiwemo mnazi, iliondolewa umuhimu wa kiuchumi, na Wapwani wakakosa mmea wa kutegemea. Wengi wametoa faida na thamani za mnazi, ambazo hivi sasa ziko kwenye kiwango cha zaidi ya asilimia mia moja ."
}