GET /api/v0.1/hansard/entries/846932/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 846932,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/846932/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ganze, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Teddy Mwambire",
    "speaker": {
        "id": 13334,
        "legal_name": "Teddy Ngumbao Mwambire",
        "slug": "teddy-ngumbao-mwambire-2"
    },
    "content": "Ninaunga mkono Hoja hii kwa asilimia mia moja. Wakati umefika wa Serikali kuangazia mmea wa mnazi ili iweze kuwafidia wakulima ambao minazi yao imeangamia. Wakulima hao wanastahili kupewa fedha ambazo zitasaidia kuendeleza ukulima wa mnazi kule Pwani na katika sehemu nyingine ambako mnazi unaweza kukuzwa. Hata katika sehemu za Ukambani kuna minazi. Kule Kisumu na katika sehemu nyingine nchini, minazi inaweza kukua vizuri."
}