GET /api/v0.1/hansard/entries/846933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 846933,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/846933/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ganze, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Teddy Mwambire",
    "speaker": {
        "id": 13334,
        "legal_name": "Teddy Ngumbao Mwambire",
        "slug": "teddy-ngumbao-mwambire-2"
    },
    "content": "Nina uhakika kwamba Serikali ikiwekeza kwenye mnazi, tutaweza kununua minazi aina ya michikichi ili tuweze kupata mafuta mengi, ambayo yatatuwezesha kuokoa zaidi ya Ksh12 bilioni, ambazo tunatumia kila mwaka kuleta mafuta kutoka nchi za nje ili tukimu mahitaji ya viwanda mbali mbali. Nina uhakika kwamba utafiti ukiendelea kufanywa kama ulivyokuwa ukifanywa katika miaka ya 2004 na 2005 – wakati Serikali ilipoangazia zaidi mmea wa Mnazi – wakazi wa Pwani wataanza kuhisi kwamba wao pia ni miongoni mwa watu katika nchi yetu ya Kenya. Ile hisia kwamba wao hawatambuliwi, na kwamba wanavumilia kuwa Wakenya, itaondoka. Wao pia watajivunia kuwa Wakenya kwa sababu kutakuwa kumetokea sababu mwafaka ya wao kuweza kupata maendeleo. Kwa hivyo, ninaunga mkono na kuwaomba Wabunge wenzangu tushirikiane na Mheshimiwa Owen Baya, ambaye ameleta Hoja hii Bungeni – na Mhe. Tayari, ambaye aliifanyia Hoja hii mabadiliko – ili tuweze kuipitisha na kuweka msukumo Serikalini ili iweze kutekeleza ombi hili ndiyo wakaazi wa Pwani, na Wakenya kwa jumla, tufaidike kikamilifu kutokana na maendeleo na tuondoe ile dhana ya kwamba tumetengwa kiuchumi."
}