GET /api/v0.1/hansard/entries/847065/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 847065,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/847065/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": " Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Mimi pia ninaunga mkono Hoja hii. Nchini Kenya tuna shida ya huo ugonjwa unaoitwa nasur kwa lugha ya mama. Ninaunga mkono ili tupate madaktari mashinani. Mambo haya ni mabaya zaidi kule mashinani kwa sababu ya ukosefu wa hospitali na madaktari wa kuhudumia akina mama ambao wako na shida hiyo. Hii ni shida kubwa kila mahali, haswa miongoni mwa jamii za wafugaji. Inakuwa aibu kubwa mpaka unaona wasichana hawaendi shuleni. Tunapochunguza tunapata wako na hiyo shida."
}