GET /api/v0.1/hansard/entries/849030/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 849030,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/849030/?format=api",
    "text_counter": 69,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia ombi hili kuhusu kahawa, chai na macadamia. Kule Pwani mazao makubwa ni korosho na nazi. Mazao haya mawili yamewekwa katika kaburi la sahau. Tulikuwa na mtambo wa korosho kule Kilifi kwa Sen. Madzayo, lakini mtambo huo umekuwa mahame sasa. Hakuna yeyote ambaye anachukua fursa hiyo kuweza kufufua mtambo ule. Vile vile, kule Kwale ambako ndugu yangu, Sen. Boy, anatoka, kulikuwa na mtambo wa Bixa, yaani ile mirangi ambayo inatumika kuweka rangi kwenye chakula ama bidhaa zingine tofauti. Tunaunga mkono ombi hili kwa sababu wakulima wengi katika eneo la Pwani wanapata shida ya soko ya korosho na nazi ilhali hayo ndio mazao ambayo yanamea kwa wingi bila juhudi kubwa ya ukulima. Tangu mazao hayo yaanze kukufa, wapwani wengi wamekuwa maskini na wameshindwa kusomesha watoto wao, kwa sababu ya kukosa ajira na fedha za kuweza kuendesha maisha yao. Tunaunga mkono ombi hili na kuomba kwamba lipanuliwe ili lihusishe pia korosho, nazi na mazao mengine yanayokuzwa nchini Kenya."
}