GET /api/v0.1/hansard/entries/851249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 851249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/851249/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kimilili, JP",
    "speaker_title": "Hon. Didmus Barasa",
    "speaker": {
        "id": 1885,
        "legal_name": "Didmus Wekesa Barasa Mutua",
        "slug": "didmus-wekesa-barasa-mutua"
    },
    "content": "Nimezipitia na nimeona ziko na dosari kidogo hasa sehemu inayosema kutakuwepo na mfuko maalum wa pesa. Ni lazima tujue mfuko huu rasmi wa pesa utaendeshwa vipi na isiwe ni njia ya kuvuja pesa ya wanachama. Vile vile, inapendekeza kuwa kutakuwa na kamati maalum ya uegezaji ambayo wanachama wake ni lazima wawe na shahada ya digri. Vile vile, inapendekeza si lazima wawe wanachama wa chama wanachowakilisha. Naona hiyo ni dosari kidogo ambayo ni lazima tuiangalie na tuzungumze na wadadisi wa masuala ya uendeshaji shughuli ya vyama vya ushirika tuone kuwa marekebisho tutakayopendekeza yawe yanalenga kuboresha sheria hizi zaidi na wala sio zile ambazo zinaendesha shughuli za vyama vya ushirika tofauti tofauti."
}