GET /api/v0.1/hansard/entries/851399/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 851399,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/851399/?format=api",
"text_counter": 318,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa nami kuzungumzia suala hili la mabadiliko katika sheria zetu na wingi wa uwepo wa sheria hizi. Nawaunga mkono wenzangu waliotangulia hapo mbeleni kusema kuwa kama tunazungumzia masuala ya mabadiliko yoyote, tunahitaji mabadiliko haya yasiwe zaidi ya sheria tano ambazo ziko hapa nchini. Hii ni kwa sababu ikiwa sheria zimejazwa tele kitabu kizima, basi Wabunge hawana nafasi na fursa ya kuweza kuangalia sheria hizi vile inavyotakikana. Mwisho Wakenya wenyewe wanakimbilia kortini kwenda kupinga mabadaliko ambayo sisi tumeyatekeleza. Ukweli ni kwamba suala linalozungumziwa hasa la kucheza michezo ya bahati nasibu na michezo ya kamari linawagusa Wakenya kwa ujumla. Hivyo basi ni sawa riba na ushuru unaotakikana kupatikana kwenye uchezaji huu wa michezo ya bahati nasibu na kamari hapa nchini uwe juu. Vilevile, Wakenya wanahitaji kupatiwa mafunzo maalum kuwa michezo hii isiwezekane kuchezwa na kila mtu hasa watoto wetu ambao wanatumia hata hela wanazopatiwa za mfukoni na hata kuchukua hela za wazazi nyumbahi kiholela ili kucheza michezo hii wakifikiria kuwa bahati yao iko kwenye bahati nasibu wakome. Suala hili linafaa kuangaliwa kwa undani zaidi na sio kwa haraka kwa sababu ni suala ambalo limezungumziwa kwa muda mrefu. Vilevile, kuna suala la maziwa. Kumependekezwa kuwa maziwa ya mbuzi na ngamia yaongezwe kwenye sheria inayosimamia halmashauri ya masuala ya maziwa. Ni sawa maana afya ya wengi waliolelewa na kutumia maziwa haya ya mbuzi na ngamia imedumishwa. Hata wazee ambao wamekuwa wakitumia maziwa haya wameweza kuishi kwa muda mrefu kwa sababu miili yao inapata nguvu za kupigana na magonjwa. Hili ni jambo ambalo halijaangaliwa kinaganaga lakini ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya waliolelewa na maziwa haya na wale wengine. Kwa hivyo kugeuza sheria hii ili maziwa ya mbuzi na ya ngamia yaweze kuwekwa katika sheria hizi ni sawa kabisa. Ningependa kuzungumzia suala la bima inayosimamia masuala ya afya hapa nchini ambayo hapo mwanzoni iliitwa bima ya kitaifa ya kusimamia masuala ya hospitali zetu. Hivi sasa Mswada huu unaweka pendekezo la kubadilisha sheria hii ili Wakenya wote waweze kuhusishwa kwenye bima hii ya afya. Jambo ambalo ni muhimu, na sisi sote tunapaswa kuangazia, ni kuwa hatutaki bodi hizi ambazo zinasimamia masuala haya kuwa kubwa mno. Tunataka bodi za kiasi na ambazo hazitakuwa na utatanishi. Lakini juu ya hayo, kuna umuhimu wa kuangalia kuwa wale wahusika na washikadau wote wamehusishwa maanake wasipohusishwa, itakuwa ni makosa kwa uamuzi kufanywa na watu wachache ambao hawataweza kuzingatia masuala ambayo yanahusisha wafanyikazi na walimu. Hao ndio wafanyikazi ambao walio wengi hapa nchini. Bima ya afya ni muhimu na inashughulika masuala ya wafanyikazi wa Serikali na wale ambao wamestaafu kazini wanaweza kuhusishwa. Kuna manufaa makubwa sana ambayo yanapatikana. Serikali zetu za The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}