GET /api/v0.1/hansard/entries/851400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 851400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/851400/?format=api",
"text_counter": 319,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "ugatuzi kama Makueni na Kitui, zimewezesha watu tofauti tofauti ambao wasiojiweza. Kuna umuhimu wa kuhusisha serikali za ugatuzi kikamilifu ili bima ya afya iwafae Wakenya na wapate huduma safi kila mahali hapa nchini Kenya. Vile vile, kuna suala la kawi na sheria zinazosimamia masuala ya kawi. Ukiangalia kwa undani, sheria hii ilikuja mwaka wa 2006 wakati ambapo tulikuwa bado hatujapata Katiba mpya. Kuna umuhimu wa serikali za ugatuzi pia zihusishwe maanake kawi haifanyi kazi hewani bali inafanya kazi kwenye maeneo ambapo serikali zetu za ugatuzi pia zipo. Ukiangalia suala la kusimamia mimea hapa nchini, kuna umuhimu wa sheria hii ihusishe bidhaa zetu zinazotoka mashambani ziwe za maana na zimfaidi mkulima. Kahawa hupelekwa nje na ikirudishwa hapa, bei yake iko juu kwa sababu haikutengenezewa hapa nchini. Hivyo basi kuna umuhimu wa kuongeza faida kwa mkulima kwa sababu faida hii ikiongezwa kwa vyakula vinavyotoka kule mashambani, bila shaka mkulima atapata faida kubwa. Halmashauri inayosimamia madawa hapa nchini inafanya kazi kwa ukaribu sana na serikali za ugatuzi. Hospitali na huduma za afya nyingi ziko chini ya serikali za ugatuzi. Sheria hii inapendekezwa ibadilishe sheria inayosimamia ugavi wa madawa hapa nchini kwenye halmashauri hii ili ifanye kazi kwa ukaribu sana na serikali za ugatuzi kwa sababu wana wafanyikazi wa kuhakikisha kuwa dawa zinazopeanwa kwa wananchi zitafaa afya ya mwananchi na hazijaletwa nchini kiholelaholela. Serikali za ugatuzi haziwezi kufanya kazi hiyo isipokuwa halmashauri hii. Pia, wakinunua dawa kwa wingi, inakuwa rahisi kwa mwanachi apate dawa na huduma zinazofaa. Masuala ni mengi lakini nikimalizia, ningependa kuzungumza juu ya kuendeleza masuala ya kukuza na kulea samaki hapa nchini. Sheria hii imekuwa tangu mwaka wa 2016. Lakini vile vile, kuna umuhimu wa kamati zinazotengenezwa zihusishe kila mtu. Nikimalizia, swala limezungumziwa hapa kuwa washikadau wote hawahusishwi katika masuala haya. Sheria zimeletwa hapa ambazo washikadau hawakuhusishwa. Katiba yetu imesema kinaga ubaga kwamba kuna umuhimu na ni lazima washikadau na umma wahusishwe katika sheria zote za nchini hapa. Itakuwaje sheria ziletwe hapa bila kuwahusisha washikadau wote? Nimesikia malalamishi kutoka kwa Wenyekiti na Wanakamati kwamba washikadau hawakuhusishwa na Wizara zinazohusika na masuala haya hazikuhusishwa. Kwa hivyo, kuna umuhimu wetu kufuata Katiba inavyosema na tusitunge sheria zetu na kuleta utapeli katika sheria tunazojaribu kutengeneza nchini ile ziwafaidi wananchi wetu. Naunga mkono Mswada huu lakini na mabadiliko."
}