GET /api/v0.1/hansard/entries/852897/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 852897,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/852897/?format=api",
    "text_counter": 52,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mumias East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Benjamin Washiali",
    "speaker": {
        "id": 151,
        "legal_name": "Benjamin Jomo Washiali",
        "slug": "benjamin-washiali"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Ningependa kuongeza sauti yangu kwa viongozi wetu wa Walio Wengi na Walio Wachache kwa kusema kwamba, tulizungumzia Hoja hii kwa urefu katika mkutano tuliokuwa nao na tukasema kwamba mfumo wa serikali iliyo sasa ni serikali ya kitaifa na serikali ya ugatuzi. Serikali ya kitaifa iko na Bunge kuu linaloangazia utendakazi wa serikali ya kitaifa. Serikali ya ugatuzi iko na Bunge lake ambalo linaangalia utendakazi wa serikali ya ugatuzi. Maoni yetu yalikua tunaweza kuzungumza lakini ni bora ikiwa tutazungumzia hospitali za umma, tuombe serikali za kitaifa na za ugatuzi kukubaliana na maoni ambayo Mheshimiwa wetu kutoka Nyali alikuwa nayo. Asante Mhe., Naibu Spika."
}