GET /api/v0.1/hansard/entries/857558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 857558,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/857558/?format=api",
"text_counter": 92,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Mheshimiwa Spika, swala la ardhi ni sugu sana katika nchi hii yetu ya Kenya. Watu wa Kaunti ya Taita Taveta wanapaswa kujua kwamba hili swala limeletwa katika Seneti. Kwa niaba ya watu wa Kwale, ambao ni majirani wa Taita Taveta, naomba, hili swala liweze kushughulikiwa kwa haraka sana. Unapotoa mwelekeo wa kutatua swala hili, ningeomba Kamati husika waende nyanjani kwenye hizo ardhi. Ilhali, wasishughulikie jambo hili wakiwa hapa. Wanafaa waende katika hizo ardhi wahakikishe na wasikize wananchi wa Taita Taveta. Nina hakika wananchi wa Taita Taveta watapata haki yao. Bw. Spika, naunga mkono ombi hili."
}