GET /api/v0.1/hansard/entries/859643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 859643,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/859643/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Nashukuru kwa kupata nafasi hii ili nizungumze kwa lugha ya kitaifa inayojulikana na Wakenya wengi hususan akina mama. Namshukuru Mhe. Duale pamoja na vinara wa Taifa la Kenya, Rais Uhuru Muigai Kenyatta, Mhe. Raila, Mhe. Ruto, Mhe. Mudavadi, Mhe. Kalonzo na wale wengine kwa sababu leo ni siku ambayo sisi kama Wabunge wa Taifa la Kenya, tutaandika historia na iingie katika kumbukumbu ya kwamba tumeheshimu Katiba yetu kwa kutekeleza matakwa yake. Ukisoma Katiba, kuna vipengele kadhaa na ibara tofauti tofauti ambazo ni wajibu wetu kama Wabunge tuzitekeleze sheria zake. Vifungu 27(3), 27(6), 27(8) vyote vinazungumuzia masuala ya usawa wa jinsia na uadilifu wa kijinsia. Zinazungumzia vipi tutaweza kuwajenga uwezo akina mama, vijana, na walemavu ili waweze kuwa na uwezo wa kufanya utetezi wao katika ulingo ulio sawa katika mambo ya kisiasa, kiuchumi, desturi zetu na mambo ya jamii. Suala hili kama tungekuwa tumeliweka katika Katiba kama tulivyoweka sheria inayohusu kaunti ama mabaraza katika kaunti zetu katika Kifungu 177, tungesema kuwa iwapo tumepiga kura na tumekuwa na asilimia zaidi ya thuluthi mbili ya jinsia moja, tutafanya uteuzi wa viongozi wengine. Tunaamini Kenya ni nchi ya demokrasia. Kuonyesha kwamba tuko na demokrasia, ni lazima katika uongozi na nyanja za kufanya maamuzi, tuwe na jinsia zote mbili. Tuwe na akina mama na akina baba. Ninataka niwambie Wabunge wenzangu kwamba wakati wa uteuzi utakapofika, hatutafanya uteuzi tu bila kufuata sheria. Katiba yetu katika Kifungu cha 100 kinazungumzia kuwa ni lazima Bunge liangalie uwakilishi wa akina mama, vijana, walemavu, makabila madogo na wale waliotengwa. Kwa hivyo, wakati tunaposoma sheria, ni lazima tuisome kwa ujumla, tusisome tu vipande vidogo vidogo. Kwa hivyo, ninataka kusema kwamba sisi kama Taifa la Kenya, tuna mikataba mingi ya kimataifa kama ile tulioandika kule Beijing, kama vile Maputo Protocol na pia ule muungano wa mataifa ya Afrika. Tuliweka mikataba kwamba tutahakikisha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}