GET /api/v0.1/hansard/entries/859644/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 859644,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/859644/?format=api",
    "text_counter": 221,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "tumekuwa na usawa wa jinsia na pia tutahakikisha kwamba akina mama wameweza kujengwa uwezo ili wapate afueni waweze kushindana sawia katika ulingo wa kisiasa, kiuchumi na hata kijamii. Sisi kama Wakenya katika Afrika Mashariki ni kama wale kaka wakubwa. Kwa lugha ya kiingereza “ the big brothers” . Ikiwa sisi ndio wakubwa, ni lazima tuonyeshe mifano bora katika uongozi na katika kuhakikisha kwamba tumeweka usawa wa kijinsia. Tukiangalia jirani yetu, Rwanda, wametupita kwa asilimia 56, Uganda asilimia 35 na Tanzania asilimia 36. Hata hapa jirani Ethiopia, juzi tu wamepata Rais mwanamke na pia jaji mkuu ni mwanamke. Haya yote ni mambo ambayo yanatuletea uwezo wa kuweka demokrasia yetu kwa usawa na kuweza kuona kwamba shabaha tunazoziweka na ruwaza ambazo tumeweka kama vile ruwaza ya 2030, akina mama wana majukumu mazito ambayo ili kuyatekeleza, ni lazima wapewe uwezo na wawe katika nafasi za kufanya maamuzi."
}