GET /api/v0.1/hansard/entries/859693/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 859693,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/859693/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu wa Spika. Mimi pia naunga mkono Mswada huu wa akina mama Kenya nzima. Ningependa kusema kwamba nilikuwa katika Mbunge la Kumi na la Kumi na Moja. Ninawashukuru wale ambao wametupatia baadhi yetu uteuzi wa kuwa katika Bunge hili. Kama Mhe. Leshoomo Maison hangeteuliwa kujiunga na Bunge la Kumi na marehemu Bi wa Taifa Lucy Kibaki, pengine akina mama kutoka jamii ya Maa hawangekuwa katika Bunge hili leo. Ninasema hivyo kwa sababu tulifunguliwa njia. Ndio maana tukapata Mhe. Peris akiwa amechaguliwa, Mhe. Naisula Lesuuda akiwa amechaguliwa, Mhe. Sarah Korere akiwa amechagula na Wabunge wengine wawili ambao wameteuliwa. Mhe. Maison Leshoomo pia alikuwa ameteuliwa ndio maana tukafunguliwa macho. Natoa shukrani kwa wanaume wote wa Jamii ya Maa, wazee kwa vijana, kwa kutuunga mkono wakijua kwamba mwanamke pia anaweza kuwa kiongozi. Ningependa wale wanaosema kuwa Wabunge wateule hawana maana wajue kwamba wana maana sana. Hii ni kwa sababu utakuwa na njia ya kujipigania. Ninawaomba viongozi wote wanaume, kila mwanamume ana mke au msichana nyumbani kwake, miaka 20 ijayo, pengine nyinyi ndio mtakuwa wachache katika Bunge hili. Kwa hivyo, Mswada huu si wa akina mama. Ni wa sisi sote. Ni wa Wakenya wote. Wale ambao watakuwa wamekosa nafasi watapata nafasi. Utanisamehe kidogo, Mhe. Naibu wa Spika. Kuna msemo - na si wimbo – unaosema kuwa: “Sisi wanawake ulimwengu mzima tuzidi kwendelea tusichoke. Mungu we, Mungu we, tusaidie. Mapenzi yote ya nyumbani juu yetu wanawake, mapenzi yote ya nyumbani juu yetu wanawake.”"
}