GET /api/v0.1/hansard/entries/859764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 859764,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/859764/?format=api",
"text_counter": 341,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "ya Kitale. Nikiwa huko, sikukaa kungoja kuteuliwa mara ya pili, nilifanya bidii kuhakikisha kwamba nimesonga kutoka kiwango hicho hadi kiwango kingine. Ndiposa unaona kwamba nimekuwa kama mwakilishi wa akina mama mara ya pili. Na vile dadangu Janet Ong’era amesema, haujui kutoka hapo, itakuwa vipi. Kama wenzetu walivyosema, tukisema jinsia hatumaanishi jinsia moja, ni yote mbili. Wakati ujao utaona kwamba huenda wanawake watachaguliwa katika Bunge hili na wanaume wenzetu wapatikane kwamba ni wachache. Hawa pia watapata nafasi ya kuteuliwa, walemavu wakiwa miongoni mwao. Ninachukua nafasi hii kumshukuru Rais, Naibu wake, Mheshimiwa Raila Amolo Odinga na Kalonzo Musyoka kwa kuamua kwa kauli moja kuwa mambo ya jinsia yakamilishwe na Bunge hili. Vile wengine wamesema, wengine wametoroka kwa sababu hawajui maana ya kusema tuwe na Mswada kama huu katika Bunge hili. Ni kwa sababu wengine wanafikiria kwamba wanawake wakichaguliwa katika nchi ya Kenya, watakuja kukalia hawa vichwani. Sio hivyo. Sisi kama akina mama, hata kwa nyumba zetu tukiwa na waume zetu hatuwakalii, tunakaa pamoja, tunasemesana na kupanga familia zetu vilivyo. Ninaamini kwamba hata katika uongozi, sisi pia tunakaa pamoja kama nyumba moja tukisemesana mambo yanayotuhusu kama familia. Ninashukuru wenzangu ambao wamejikakamua hadi wamerudi hapa mara ya pili. Vile wamesema, matusi sio hapa tu. Vile wenzangu wanasema, matusi hata kule nje yako. Mimi ninakumbuka Mhe. Wanga wakati alitaka kuwa mwenyekiti wa ODM. Niliskia matusi ikitoka kwa wenzetu hapa wakisema huyu hawezi lakini ninaona ni mchapa kazi. Ninajua kwamba kuanzia hapo kusonga mbele, Mhe. Wanga atapata nafasi ya juu. Hata katika kanisa, zamani watu walikuwa wanaamini kwamba wahubiri lazima wawe watu wa kiume lakini wakati huu, hata sisi pia wanawake tunaweza kuwa wahubiri. Ninaunga mkono na ninaomba wenzangu waunge mkono. Asante."
}