GET /api/v0.1/hansard/entries/859803/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 859803,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/859803/?format=api",
"text_counter": 380,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Catherine Waruguru",
"speaker": {
"id": 13253,
"legal_name": "Catherine Wanjiku Waruguru",
"slug": "catherine-wanjiku-waruguru"
},
"content": " Naomba kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili nikiungana na Wabunge ambao wamezungumza mbele yangu. Mmoja wao Mhe. Mishi Mboko ambaye alisema wamama wetu hata wale ambao hawakuingia darasani ni Wakenya, wanalipa ushuru na pia tunatembea katika hii safari pamoja na wao. Niruhusu kwa njia ya kipekee niseme asante kwa Mhe. Aden Duale na uongozi wa hii nyumba ya kitaifa. Pia kwa Mhe. Rais Uhuru Muigai Kenyatta kwa kukubaliana na sisi, na kuomba Wakenya wote wakubaliane na huu mwito wa Two-Third Gender Bill, umefika wakati wa kutekelezwa. Natuma asante zangu pia kwa Deputy President, Mhe. Raila Odinga, Mhe. Kalonzo Musyoka, Mhe. Mudavadi na Mhe. Wetangula pamoja na Wizara ya Gender ambao wamesimama na sisi. Pia washikadau wengine ambao wametoa rasilimali zao, wamama na viongozi wa kiume ambao wamesimama na sisi kwa kutayarisha huu Mswada ndio ufike hapa. Pia niruhusu niseme kwa njia ya kipekee kwamba Wakenya wako na matarajio mengi sana katika hii Bunge ya 12. Nikisema hivyo, najua Wabunge ni wanasiasa. Wanajua zile changamoto ambazo sisi kama viogozi tunapitia. Moja yake ni propaganda ambazo hutumiwa kupiga jambo lolote ambalo Wakenya hukubaliana nalo. Lakini, niruhusu tu ni kumbushe wananchi wa Kenya kwamba Mhe. Mwai Kibaki, zile enzi wakiwa na Mhe. Raila Amollo Odinga wakati alikuwa Waziri Mkuu, waliweza kutembea katika sehemu zote za Kenya wakiuliza Wakenya watoke kwa idadi kuu kupiga kura ya Katiba ya mwaka 2010 na wakafanya hivyo. Hii ndiyo iliweza kutupatia jambo hili ambalo tunazungumzia la thuluthi mbili. Hii thuluthi mbili si ya akina mama peke yao ni ya jinsia zote. Hii imekuwa safari ambayo mwaka mmoja uliopita Bunge la Taifa tulijiahidi kwamba tutaweza kutekeleze huu mjadala na pia kutunga sheria lakini haijawezekana. Tunavyoongea katika mkono ule mwingine wa Serikali ambao tunauita mahakama wako na matarajio na sisi. Tukifanya hivyo, tutaokoa pesa ambazo zinaweza kutumika kwa sababu ya mambo ambayo yanaafikiana na kutotii sheria na Katiba ambayo kila mmoja wetu aliapa na kusema atailinda, ataihifadhi na kuitunza. Na tuliapa kwa Quran na Bibilia. Nazidi kuomba ndugu zetu wanaume na pia wamama kwamba wiki ijayo tutoke kwa idadi kuu manaake tumeongea na mimi najua yule ambaye alitilia maanani lile jambo ambalo tumezungumza siku ya leo. Hakuna kitu kingine kimebaki kwetu kufanya ila kuwaomba tutoke kwa idadi kuu. Nimeona kwa mtandao Mbunge dada yangu Mhe. Gathoni wa Muchomba, Gladys Wanga na mimi kama tumechorwa sura maridadi lakini mdomo ni wa yule mnyama anaitwa nguruwe. Wabunge wanaitwa Mpigs, sijui kama ni jina la Mpesa walikosea. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}