GET /api/v0.1/hansard/entries/862879/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 862879,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/862879/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Changamwe, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Omar Mwinyi",
    "speaker": {
        "id": 1345,
        "legal_name": "Omar Mwinyi Shimbwa",
        "slug": "omar-mwinyi-shimbwa"
    },
    "content": "inaonyeshwa moja kwa moja katika vyombo vya habari, mashahidi wengine pengine waliona kuna hatari na wakija pale katika Kamati wakasema: “Sisi hatukuona na hatukusikia.” Sasa kama mtu ashasema hakuona wala hakusikia, hakuna mahali ambapo tungeweza kusonga mbele. Vile vile, katika Ripoti hii, tumeona kwamba iko haja ya Bunge hili lijichukue kama Bunge la kitaifa. Ripoti ambayo inakuja hapa iangaliwe kwa mujibu wakitaifa na tusione kwamba ni Wabunge wa magharibi peke yao ndio wanafaa kuchangia mambo ya sukari na wengine wawe wanapinga. Jambo la haki liwe la haki. Katika Ripoti hii tumeona kwamba kumekuwa na bidii na juhudi za kuwa Hoja hii iangushwe kwa sababu kulikuwa na mawaziri ambao walikuwa lazima wakingwe wasije wakaumia. Nafikiri huu si mwendo ambao Bunge hili lafaa kuchukua. Ikiwa twataka kukomesha ufisadi, kila mtu ambaye atakuwa ametajwa apewe nafasi aweze kuulizwa na yeye mwenyewe aweze kujisafisha. Hivyo tungeweza kukomesha mambo ya ufisadi katika nchi yetu. Hata jana katika Bunge la Seneti, walikuwa wakijadili mambo ya Ruaraka, tuliona bado kuna watu walikuwa wanakingwa katika Ripoti hiyo. Nafikiria mwendo huu ukiendelea, itakuwa sisi kama Bunge hatutekelezi kazi yetu sawa sawa. Mwisho, napenda kuangazia maombi yetu katika Bunge hili. Kabla hatujaanza kikao chetu huwa tunasema: “Ewe Mwenyezi Mungu, ambaye kwa hekima na wema wako umeteua nyadhifa za viongozi na mabunge kwa ustawi wa jamii na utawala wa haki wa wanadamu: twakusi hi ututazame kwa neema nyingi sisi watumishi wako, ambao umeridhika kutuita ili tutekeleze shughuli muhimu za Jamhuri hii yetu.” Mhe. Naibu Spika wa Muda, hili ni moja katika mambo ambayo twatakiwa tuyazingatie. Mwisho kabisa, ombi hilo linasema:“Twakuomba ututeremshie Baraka zako sisi tuliokutanika hapa…” Kisha inamalizia ikisema: “…ufanisi na heri ya nchi hii yetu na wale ambao haja zao umezikabidhi mikononi mwetu.” Ikiwa wananchi wametukabidhi sisi majukumu yakuangalia maslahi yao na mambo yao yaende sawa sawa, itakuwa hatutekelezi kazi zetu ikiwa tutaenda kinyume chao."
}