GET /api/v0.1/hansard/entries/865012/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 865012,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/865012/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kitutu Chache South, FORD-K",
    "speaker_title": "Hon. Richard Onyonka",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Ni heshima kusikiza Mzee Angwenyi akizungumza katika Bunge hili kwa sababu ni mzee tunayemheshimu sana. Mimi binafsi, ni mzee ambaye nimemjua na nimefanya kazi naye. Ningependa kusema kuwa ametupatia busara na masuala ambayo ameyazungumzia ni ya kiheshima. Jambo la kwanza ningependa kusema ni kwamba waandishi wa magazeti nchini Kenya wamechukua liwe jukumu lao kila wakati kuzungumzia mambo ya Bunge hili lakini wakiandika habari kuhusu Bunge hili zinakuwa za kupotosha kila wakati. Nafurahi kwa sababu ndugu zangu ambao wamezungumza wamesema kuwa tungependa waandishi wa magazeti wakiandika kama ni hela ambazo tunapewa kununua nyumba waseme kuwa nyumba hiyo ni lazima tuilipie kwa miaka mitano na ni pesa ambazo zinachukuliwa kutoka kwa mshahara wangu. Mshahara wangu ni Kshs640,000 lakini pesa za kulipia nyumba hii ni Kshs600,000. Kila Mbunge lazima atoe mshahara wake wote ndio anunue nyumba. Sisi tunasema tungependa tulipiwe mahali ambapo tunaishi. Kwa kizungu tunaita house allowance . Kama mfanyakazi wa serikali yoyote, sisi tuwe na uwezo wa kuishi. Jambo la pili nitakalosema ni ukiangalia Tume ya Huduma za Mahakama (JSC), jaji anapewa nyumba, gari na bima. Tungependa kusihi kuwa nasi pia masuala haya yaangaliwe. Kumalizia, ningependa kumsifu ndugu yangu, Mhe Junet Mohamed, ambaye ameleta jambo hili tunalolizungumzia. Ningependa kumsifu ndugu yangu, Mhe. John Mbadi, ambaye amelizungumzia jambo hili. Ningependa kusema kuwa sisi tungependa kufanya kazi nzuri hapa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}