GET /api/v0.1/hansard/entries/865135/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 865135,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/865135/?format=api",
"text_counter": 301,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif, Athman",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka nikubaliane na Kiongozi Wa Wengi Bungeni kwamba hili jambo tayari liko kwenye Katiba yetu. Vile nakubaliana na yule aliyeleta kutaka kurekebisha haya. Ukweli ni kwamba, matatizo juu ya maswala haya yapo. Pesa zinatengwa na Bunge; zina kwenda kwa wizara; kandarasi inatangazwa; anayefanya kandarasi ile inatia sahihi makubaliano ya kandarasi. Lakini ajabu ni kwamba, ikifika wakati wa malipo, linakuja swala lile kwamba hakuna pesa. Si serikali ya kaunti, ama Serikali ya uma. Kuna mkandarasi anadai pesa. Amefanya kazi takriban miaka miwili na alitia sahihi maafikiano na hajalipwa pesa: Anaambiwa hakuna pesa."
}