GET /api/v0.1/hansard/entries/866369/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 866369,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/866369/?format=api",
    "text_counter": 439,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Bura, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Wario",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwanza kabisa, nimesimama kuunga Mswada huu mkono. Pia, nachukua fursa hii kushukuru Kiongozi wa Wengi Bungeni kwa kuleta Mswada huu ambao ni muhimu kwa taifa na watu wa Kenya kwa jumla. Sheria iliyo mbele yetu ina vifungu 64, sehemu nane na ratiba ama schedule nne. Lengo na maudhui ya sheria hii ni nini? Ni kwa sababu tunataka kufuta Kifungu 208 yaani National Youth Service (NYS) Act tuibadilishe ili tulete sheria ambayo inaambatana na Katiba 2010 na inaweza tatua matatizo yanayokumba taasisi ama shirika la NYS. Historia ya taasisi ya NYS inasikitisha. Watu wachache wameshirikiana kuwa wafisadi na kudhulumu vijana ambao tumewatuma wasome. Wameenda kuiba pesa. Hii ni hali ambayo imeleta huzuni na kueleweka vibaya kwa NYS katika taifa la Kenya na wananchi kwa jumla. Hali hii imeadhiri utendakazi, hadhi na jina la NYS. Tutafanya nini kama Bunge na taifa ili hadhi, heshima na jina la NYS lirudi pale lilipokuwa zamani? Mwizi ni nani? Ni nani ameiba pesa za umma? Je, ni watoto 15,000 tuliowatuma kujifunza? La, sio wao. Mara hii, hatua imechukuliwa kwa waliohusika kuiba pesa za umma. Nashukuru kwa sababu wako mahakamani. Kwa hivyo, hakustahili kuuwawa kwa taasisi ya NYS kwa sababu ya makosa ya watu wachache. Wale watoto ambao wanaenda kupata mafunzo hawana hatia. Wanafanya juhudi na wajibu wa kujenga taifa la Kenya. Hawastahili kubeba mzigo wa wale walioenda kuiba pesa za NYS. Katika hii sheria, lengo kubwa ni kubadilisha muundo ili mara hii kuwe na baraza. Alivyosema Kiongozi wa Wengi Bungeni ni ukweli kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}