GET /api/v0.1/hansard/entries/866370/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 866370,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/866370/?format=api",
    "text_counter": 440,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Bura, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Wario",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "sababu NYS ilikuwa inaanza na Director-General na inaisha na yeye pia. Tunaleta baraza leo ambalo litaangalia hali ya utendakazi wa NYS. Kama kuna ufisadi, baraza lile litakuwa la kwanza kupiga parapanda na kuita Wakenya na kuwajulisha ya kwamba hali haiko sawa huko. Kwa hivyo, tumesema tubadilishe muundo wa NYS. Pili, kwa furaha kubwa, nafurahi na kumpongeza Rais kwa kuleta mabadiliko katika uongozi wa NYS. Moja, ameleta Principal Secretary Owino ambaye ametoka mashinani. Alikuwa kama ofisa wa tarafa. Amepanda mpaka mahali ako leo. Ni mtu ana ujuzi na imani kuona kwamba shirika la NYS linaenda mbali. Bwana Matilda Sakwa ambaye ni Director- General wa NYS ni mtu amesimamia taasisi ya umma kwa muda mrefu. Kwa hivyo, tukibadilisha viongozi wa taasisi hii na tuwe na sheria mpya, kwa hakika, lengo la kuwa na taasisi ya NYS inayotoa mafunzo kwa watoto wetu tutaifikia karibuni. Vijana 15,000 walimaliza masomo katika NYS juzi. Kwa sababu ya ufisadi katika NYS, Kamati ya Bajeti imepunguza zaidi ya Ksh.6milioni ya shirika hiyo. Wale watoto wanaoenda pale kusoma wanataka chakula, matibabu na rasilimali. Pesa ile imetolewa imepelekwa kwa barabara. Hii si haki wala si sawa. Kwa mujibu wa Kifungu 118 cha Katiba 2010 na Kifungu 127 cha Kanuni za Bunge, tulialika Wakenya kwa jumla. Walikuja wananchi wa tabaka na taasisi mbalimbali, ikiwemo Kenya Law Reforms na wizara, wakatoa rai zao ambazo tumeweka katika Ripoti. Mtasoma ili ituwezesha kurekebisha sheria iliyo mbele yetu kwa manufaa ya taasisi, vijana na taifa la Kenya kwa jumla. Kabla sijasahau, ningependa kuchukua fursa hii kushukuru Kamati ya Kazi na Maslahi ya Jamii. Wamechukua muda mrefu kupitia Vipengele 64, moja baada ya nyingine. Tulizungumza mpaka saa zingine tukachoka tukijadili ili kuweza kuafikiana na kutoa sheria kwa taifa la Kenya. Naomba Waheshimiwa Wabunge kwamba NYS sio wezi, wezi ni watu ambao wameenda pale na wameshirikiana na viongozi wa hiyo taasisi ili kudhulumu watoto wetu. Ni haki tubadilishe sheria ili vijana wapate mafunzo pale ili wahudumie taifa la Kenya. Ombi langu kwa Waheshimiwa Wabunge ni wapitishe hii sheria ili tuweze kuhudimia Wakenya. Kwa hayo machache, Mhe. Spika wa Muda, naunga mkono sheria hii. Asante."
}