GET /api/v0.1/hansard/entries/86659/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 86659,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/86659/?format=api",
"text_counter": 59,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Joho",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 30,
"legal_name": "Hassan Ali Joho",
"slug": "hassan-joho"
},
"content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika. Tunazungumzia maisha ya binadamu katika Bunge hili. Maisha ya binadamu yana haki ya kulindwa na Serikali ya nchi hii. Sisi, kama wawakilishi, tunahaki ya kuwakilisha matakwa ya wananchi wa Kenya. Nimeshtuka kumsikia Waziri Msaidizi akisema kwamba maisha yanapopotea inakuwa ni jambo la kuzungumzia tu, na kusema ânitachunguzaâ. Ninayajua maeneo ya Kisauni, ambayo ninawakilisha Bungeni. Watu wasiopungua kumi walipoteza maisha yao. Hakuna uchunguzi uliofanywa, isipokuwa nimemsikia Waziri Msaidizi akizungumza kwa nguvu na hamasa kwamba watafanya uchunguzi. Ningependa kumuuliza Waziri Msaidizi atoe list ya watu ambao wameuawa katika miezi sita iliyopita, ni wangapi ambao mauaji yao yamechunguzwa, na ni watu wangapi waliopelekwa kortini na haki kutendeka?"
}