GET /api/v0.1/hansard/entries/866655/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 866655,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/866655/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kimilili, JP",
"speaker_title": "Hon. Didmus Barasa",
"speaker": {
"id": 1885,
"legal_name": "Didmus Wekesa Barasa Mutua",
"slug": "didmus-wekesa-barasa-mutua"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii pia kuunga mkono Ripoti ya Kuratibisha Itifaki ya Afrika Mashariki kuhusu Mawasiliano na Tecnolojia ya Habari. Teknolojia ni muhimu sana kwa sababu itarahisisha mawasiliano miongoni mwa watu ambao wanaishi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikikisiwa kuwa na pendekezo kwamba tunataka tuwe na Jumuiya ambayo haina mipaka. Nafikiria mawasiliano ni kitu cha muhimu sana kwa sababu yatarahirisha mawasiliano ya simu za rununu na vile vile kuhakikisha kwamba operasheni za polisi hasa kufuatilia majangili pia zinategemea huduma za mawasiliano. Tumekuwa na wakora ambao wamekuwa wakizunguka katika nchi za Afrika Mashariki. Kwa hivyo, itakuwa rahisi sana kwa polisi wa Kenya kuwafuatilia wakora ambao wamekuwa na mazoea ya kuiba magari wakienda kuyaficha katika sehemu ambazo hazina ubora wa mawasiliano. Vile vile, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuna usafirishaji wa bidhaa muhimu kutoka Mombasa kuelekea mataifa ya Rwanda, Uganda na Tanzania ambayo pia lazima wenye mizigo wafuatilizie kwa kimombo ikijulikana kama tracking . Hii itarahisisha huduma hiyo muhimu sana kwa sababu bidhaa za bei ghali lazima zifuatiliwe na teknolojia. Inasemekana kwamba kuna pendekezo moja la idara ya forodha ambalo linasema kwamba lazima uweze kufuatilia mizigo uhakikishe kwamba haupotei ama magari ambayo yamekisiwa kupelekwa Uganda yasije yakatumiwa hapa nchini, jambo ambalo litafanya Kenya kupoteza ushuru. Kwa hivyo naunga mkono kwa sababu mawasiliano ni nguzo ya uchumu na uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utategemea ratiba hii ya itifaki ya Afrika Mashariki. Juzi nilipita katika Eneo Bunge la Mhe. Babu Owino na nikaona kwamba alikuwa na mpango wa kuweka sehemu fulani ya mawasiliano ili watu wa Embakasi Mashariki wawe na urahisi wa kutumia intaneti na mambo mengine. Kwa hivyo, kwa upande mmoja, nafikiria sio eti Mhe. Babu alikuwa hataki bali alikuwa anasema kwamba hii ni muhimu na labda itafuatiliziwa katika mambo muhimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mhe. Naibu Spika, naunga mkono."
}