GET /api/v0.1/hansard/entries/866811/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 866811,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/866811/?format=api",
"text_counter": 313,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ali Sharif",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Kama tunavyofahamu, ulimwengu wa leo umebadilika kwa namna nyingi sana, ndiposa fikira hii imefika mahali pa kwamba ni muhimu sana kwa Serikali kuhakikisha kwamba wameweza kulitekeleza jambo hili punde tu tutakapolipitisha hapa Bungeni. Leo hii mambo mengi yanavyoendeshwa ulimwenguni kwa ujumla yanatumia mitandao katika kupata zile habari ama kutuma habari zozote zinazohusiana na mambo ya kileo. Lakini kwa masikitiko makubwa katika sehemu nyingi sana katika nchi hii, utapata kwamba mambo kama haya hayapatikani. Utapata sehemu nyingi sana wanatumia zile teknolojia za zamani katika kuwasiliana na mambo mengi sana ama kuweza kufanya zile shughuli zao za kileo. Ukweli ni kwamba sio kwamba vijana pekee watafaidi katika Hoja hii, wao tu ni miongoni mwa wale watakaofaidi sana. Lakini ni jambo litakaloinua uchumi wetu na kuendesha harakati za mambo yetu kama vile nchi nyingine zinafanya. Walimu wanahitaji kutumia huduma kama hizi katika sehemu za mashinani lakini hazipatikani. Inawabidi kusafiri kwenda sehemu nyingine ambazo kuna huduma hizi ama kugharamika pakubwa katika kuzipata huduma hizi."
}