GET /api/v0.1/hansard/entries/866812/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 866812,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/866812/?format=api",
    "text_counter": 314,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Ningependa kuunga mkono na kuhimiza ya kuwa lifanyiwe haraka jambo hili na litekelezwe kikamilifu. Jambo ambalo singependa lipatikane ni kwamba watashirikishwa waezekaji wa kibinafsi. Kama tutafanya hivyo, basi, itakuwa bado hatujasonga mbele. Leo hii waekezaji wa kibinafsi wanaweza kufanya huduma hii katika sehemu ambazo hamna, lakini tunapolijadili hapa, huwa tunapendekeza Serikali ichukue majukumu haya kwa sababu matatizo yale ambayo tunayahofia sasa hivi, walioko mashinani hawapati huduma hizi. Hata kesho zikifika huduma hizi na ikiwa wameshirikishwa hawa waekezaji wa kibinafsi gharama zitakuwa vile vile. Kwa hivyo, ningependa Serikali iingilie kikamilifu na kuhakikisha wametekeleza huduma hii kwa Wakenya wengi. Asante."
}