GET /api/v0.1/hansard/entries/867307/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 867307,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/867307/?format=api",
    "text_counter": 193,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwatate, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Mwanzo kabisa, nasimama kuunga mkono marekebisho haya. Kilimo ni miongoni mwa sekta ambazo ziko rohoni mwa majimbo yote ya Kenya. Ugatuzi ni kitu ambacho Wakenya walipigania na tumeona maendeleo ya ugatuzi. Ingawaje kuna madoadoa hapa na pale kwa sababu ya rushwa, ugatuzi bado umewasaidia Wakenya wengi isipokuwa mfumo wa ugavi wa huu mgao ambao tunatumia sasa hivi kidogo uko na dosari. Nikiangalia, kuna majimbo kutoka tangu tupate Uhuru mwaka wa 1963 ambayo bado hayana maji na ukiangalia katika majimbo mengine, wana maji yakutosha yakunywa na yakufanya unyunyizaji mashambani mwao. Wengine hata yakunywa ni matatizo. Mfano ni kule kwangu Mwatate ambako maji ya kunywa ni tatizo. Maji mengi ambayo yanachimbwa kwa visima, kwa sababu ya madini, hayako masafi kwa wananchi kuyatumia. Ugavi uko na tatizo katika majimbo yetu. Naomba Seneti ijaribu kuangalia na kubadilisha mfumo wa ugavi. Tukisema eti mahali kuna idadi kubwa ya watu ndio hela zinaelekea nyingi… Kuna majimbo ambayo yana watu kidogo lakini ni makubwa na barabara ni zilezile. Sasa ukiwapatia hela kidogo, utaona kwamba majimbo mengine yanaendelea zaidi kuliko mengine."
}