GET /api/v0.1/hansard/entries/867308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 867308,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/867308/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mwatate, ODM",
"speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Sasa hivi nilikuwa na angalia rununu yangu. Ukiniruhusu nitadokeza kuhusu niliyoona katika WhatsApp . Mmoja amesema: “Usifananishe maendeleo ya Taita Taveta na Kaunti ya Kitui. Usitofautishe maendeleo ya Taita Taveta na Kaunti ya Kwale.” Lakini ukiangalia ugavi wa Kwale na ule wa Kitui ni mkubwa kuliko ule wa Taita Taveta. Kwa hivyo, huwezi kufananisha maendeleo ya majimbo haya na majimbo mengine ambayo yanapata hela kidogo, haswa Taita Taveta maana jimbo ni kubwa na linataka hela nyingi. Mfumo ungetengenezwa ikawa kwamba kama ni dawa, mahali kuna watu wengi basi Seneti ingetengeneza kwamba jimbo ambalo lina watu wengi lipelekewe pesa nyingi za dawa lakini kama jimbo ni kubwa, kwa mfano, katika upande wa barabara na lipewe hela nyingi kuliko majimbo mengine, hapo ndipo kuna tatizo. Ukweli ni kwamba kuna maendeleo maana tumepiga hatua mpaka sasa hivi. Kila jimbo Kenya liko na kilimo. Kwa hivyo, kuboresha kilimo ni sawa na kuboresha maisha ya Wakenya."
}