GET /api/v0.1/hansard/entries/868024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 868024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/868024/?format=api",
    "text_counter": 23,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": " Mhe.Naibu Spika, naomba kutoa azimio la Hoja ifuatayo: KWAMBA, tukitambua kuwa Ibara ya 43 ya Katiba imebainisha kila mtu ana haki ya kupata kiwango bora zaidi cha afya kinachojumuisha haki ya kupata matunzo ya kiafya na kutonyimwa matibabu ya dharura; aidha ikifahamika kwamba gharama za matunzo ya kitabibu katika taasisi za kiafya za kibinafsi zingali ghali mno, hivyo kuwalazimu Wakenya wengi kupendelea kusaka huduma hizo kwa hospitali za umma; tukizingatia kwamba licha ya bei nafuu ya matibabu katika hospitali za umma ikilinganishwa na hospitali za kibinafsi, bado Wakenya wengi hawamudu, hivyo basi kutumbukia kwenye madeni, ufukara na dhiki wanaposhindwa kulipa malimbikizi ya gharama za matibabu yao na ya wapendwa wao; Bunge hili linahimiza Serikali ya Kitaifa kufutilia mbali gharama zote za matibabu za wagonjwa wote wanaofariki wakipokea matibabu katika hosptali za umma za rufaa. Asante, Mhe. Naibu Spika."
}