GET /api/v0.1/hansard/entries/868853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 868853,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/868853/?format=api",
    "text_counter": 284,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Vile vile, tumeshuhudia mara nyingi sana nchi hii ikilalamika kuhusiana na masuala ya uchumi na matatizo mengineo. Naamini pakubwa haya yanasababishwa na hali ya kutodhibiti kile tunachopata kwa uangalifu. Asilimia 25 ambayo inaenda kwa kaunti sio pesa kidogo. Lakini utapata ya kwamba pesa hizi zinazoenda kwa kaunti, kaunti nyingi bado zinalalamika kuhusiana na miradi na maendeleo. Naamini pakubwa kwamba kama utaratibu huu ambao tuaujadili hapa utaweza kutumika kiusawa, nina imani kwamba matatizo kama haya hayatashuhudiwa mbeleni. Ukweli ni kwamba nchi hii ina umuhimu mkubwa wa kuhakikisha ya kwamba fedha za umma zimedhibitiwa na zimetumika kiusawa na kiuangalifu."
}