GET /api/v0.1/hansard/entries/868855/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 868855,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/868855/?format=api",
    "text_counter": 286,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Vile vile, mbali ya kwamba tunayazungumzia haya leo ama tunayajadili marekebisho haya, ni lazima tukubali matatizo yako na ni sisi tunayasababisha kupitia serikali za kaunti ama Serikali Kuu. Utapata kwamba utaratibu huu ambao tunaujadili hapa, wengine wanautumia kama sababu kwa mambo yao ya kibinafsi. Mfano ni namna serikali za kaunti zinavyotaka kutumia pesa zao. Lakini hapa katikati, hofu ni kwamba kuna baaadhi ya Wakenya ambao ni wahusika katika kutumia utaratibu huu. Wanatumia mbinu za kusikitisha badala ya kufanya mambo kiutaratibu hasa kwa kuzingatia mwongozo huu ambao tunazungumzia. Kuna miradi ambayo inahitaji kufanywa kila mwaka lakini hucheleweshwa kwa sababu ya mwongozo ambao tunaotumia. Wale ambao wanahusika katika kuendesha haya mambo… Ikiwa tunaipenda nchi hii na tunataka haya tunayozungumza yawe ni mambo ya usawa na ukweli sharti tuhakikishe The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}