GET /api/v0.1/hansard/entries/868857/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 868857,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/868857/?format=api",
"text_counter": 288,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Magavana tunawajua. Sifa za wengi wao zinajulikana. Siyo wote wenye sifa za kupendeza. Udhaifu upo ndani ya baadhi ya ndugu zetu. Kutokana na hali hii ambayo tunajadili sasa hivi, ni vyema kuhakikisha kwamba mwongozo huu umewekwa vikwazo vya kisheria namna inavyotakikana. Hivyo, tutahakikisha kwamba yeyote ambaye ni mhusika katika kaunti ni mhusika wa kuendeleza kaunti. Masuala ya fedha yatadhibitiwa kwa njia ya furaha kubwa. Serikali ya kitaifa yafaa kuhakikisha kwamba imepeana mwongozo kwa serikali za kaunti kuhusu matumizi ya fedha. Tumeshuhudia mara kadhaa matatizo katika kaunti tofauti tofauti. Mimi naona yamesababishwa na hali ambayo haikuwa hapo mbeleni ya kuweka utaratibu mwafaka wa kudhibiti hizi fedha za umma. Ninaunga mkono marekebisho haya. Nawasihi wale wahusika wote katika jambo hili wahakikishe kwamba kuna mwongozo wa kujua kwamba hizi ni fedha za umma na zinahitaji kutumiwa kwa njia ya kuwanufaisha Wakenya. Sharti kila kitu kiwe mahali pake. Wale ambao wamepewa nafasi wasigandamize wengine kwa kutumia mbinu za kusambaratisha mambo. Wasiingize maono yao ya kibinafsi. Mhe. Spika, ningependa kukomea hapo na kuunga mkono haya marekebisho. Fedha za umma zahitaji kuangazwa kikamilifu."
}