GET /api/v0.1/hansard/entries/872802/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 872802,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/872802/?format=api",
    "text_counter": 415,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "kwamba pesa za wafanyikazi zimewekwa mahali ambapo kila wafanyikazi wanapofanya kazi na ikifika wakati wa kustaafu, wanaona pesa zao ziko katika hali madhubuti na wanaweza kuzifikia, kuzitoa na kuzitumia. Jambo la kuaibisha zaidi ni kwamba, kumekuwa na majabali wawili wakipigana kuhusikana na mambo haya ya pesa za wafanyikazi za kustaafu. Na sijui ilikuwaje wakati huu ikaonekana kwamba Mswada huu ni lazima uanzie katika Bunge la Kitaifa. Jambo hili ni makosa makubwa. Niliweza kulisema jambo hili na kuliweka wazi katika Kamati yetu. Ninashukuru ndugu yangu Mwenyekiti yuko hapa. Nilipinga sana na nikasema si haki kwa Mswada huu kuanzia katika Bunge la Kitaifa. Mswada huu ni lazima uanzie katika Bunge la Seneti."
}