GET /api/v0.1/hansard/entries/872803/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 872803,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/872803/?format=api",
"text_counter": 416,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Lakini kama tunavyoelewa, wakati ule kulikuwa bado hakuna handshake . Kwa hivo ilikuwa ‘wengi wape’. Na ikapita ikaendelea. Leo tunajadili Mswada huu ukiwa ulipitishwa na Bunge la Kitaifa kisha kuletwa hapa. Sisi ni kama ambao tumeambiwa ‘jadilieni yale yaliyoko sasa.’ Wafanyikazi katika kaunti zetu ni binadamu kama sisi. Wanaweza kucheleweshwa malipo yao ya kustaafu ama ya uzeeni. Utakuja kuona ya kwamba, wakati wa kustaafa, utashangaa kama mtu huyu alifanya kazi hapo awali ama hakufanya kazi kabisa, kwa sababu atakuwa amecharara na hali yake ya maisha ya baadaye yanakuwa mabaya sana. Watoto wake pengine hawataendelea na masomo kwa sababu ya ukosefu wa karo. Wakati mwingine mabibi wao wanawatoroka na wanaishi maisha ya upweke. Mswada huu ni muhimu sana kwa Bunge hili la Seneti. Tunahitajika kujadiliana na kutafakari kwa undani sana ili tuweke matakwa ya wafanyikazi wa kaunti mbele wanapostaafu. Wakati huo, watoto wao watakuwa wameajiriwa kazi kwa sababu watakuwa na umri wa zaidi ya 20. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba watakapostaafu wapate pesa zao bila matatizo yoyote. Ikiwa mtu atastaafu, basi apewe haki yake mapema ili pesa hizo zimsaidie katika maisha yake ya baadaye. Pesa hizo zitamsaidia kupata matibabu anapogonjeka, kuwaelemisha watoto na wajukuu na pia kujikimu kimaisha kama watu wengine. Jambo la kusikitisha ni kwamba tuna ndovu wawili wanashindana. Lakini kama walivyosema hapo awali, wakati huu ni muhimu tuweke nafsi zetu kando tuone ya kwamba huu Mswada umepita ili wafanyikazi wa kaunti zetu wafaidike. Kwa sababu hapa tusiweke nafsi zetu binafsi halafu zinaleta mtafaruku fulani ili Mswada huu usiweze kujadiliwa. Wakati huu, hakuna kurudi nyuma. Mswada huu lazima ujadiliwe hapa. Kuna ndugu yangu hapa, Mwenyekiti wa Kamati ya Wafanyikazi, na ni sharti aone ya kwamba ikiwa sisi tulisema tutajadiliana na kukubaliana kama vile tulivyoafikiana ndani ya Kamati, kwamba ijapokuwa wameuleta Mswada huu hapa, tutaujadili vilivyo. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu. Ni lazima tujadiliane na tukubaliane wakati huu, usiwe tena na mtafaruku wa aina yoyote. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}