GET /api/v0.1/hansard/entries/872812/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 872812,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/872812/?format=api",
    "text_counter": 425,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sakaja",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13131,
        "legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
        "slug": "johnson-arthur-sakaja"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda. Nitajibu kwa Kiswahili. Ningependa kumweleza Sen. Madzayo ya kwamba, sikuwa na shida wala hoja ya nidhamu wakati Sen. Halake alisimama. Ilikuwa ni kumpa maelezo zaidi. Katika Bunge la Seneti tuko na shida kwa sababu Mswada huu ulikuwa ushajadiliwa hapa na tukaupitisha, ilhali ulianzishwa tena katika Bunge la Kitaifa. Lakini ukiangalia yaliyomo ndani ya Mswada huu ni sawa na yale tuliyoyapitisha. Nilikuwa nampa maelezo zaidi. Mswada huu umeletwa na Kiongozi wa Walio wengi na sio Mwenyekiti wa Kamati. Kwa hivyo, sitakuwa na nafasi baadaye ya kujibu."
}