GET /api/v0.1/hansard/entries/872847/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 872847,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/872847/?format=api",
"text_counter": 460,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kwa hivyo, tusifichane kilugha hapa; tuambiane wazi wazi iwapo Mswada alio nao ataendelea nao, ama atauwacha. Halafu tuangalie tutashika lipi na tuache lipi kuliko kuleta mkanganyiko. Hivi sasa, kuna Mswada unaozungumziwa katika Bunge la Kitaifa, na pia kuna mwingine unaozungumziwa hapa katika Bunge la Seneti, na hiyo sio sawa. Iwapo tutafanya hivyo, lazima tuzingatie kwamba ndovu wakipigana, nyasi ndizo huumia. Hapa tunaendelea kupigana sijui ni Bunge la Kitaifa, na Bunge la Seneti; tunagombana kwa sababu ya pesa za wafanyakazi. Wanaoumia hapa ni wafanyikazi. Hatukuletwa hapa kuonea wafanyakazi; tuliletwa hapa kuwasaidia wafanyikazi na sheria. Hii sio haki! The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}