GET /api/v0.1/hansard/entries/873839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873839,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873839/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": "Nitaanza mjadala wangu kwa kulitaka Bunge hili, kuweza kutunga sheria ya kufutilia mbali ada dhidi ya maiti. Hii ni kwa sababu tunajua wazi ya kwamba huwezi dai maiti. Kwa nini nasema tuweze kufutilia mbali ada hizi? Nina sababu zangu ambazo niliweza kupata baada ya kuzunguka mashinani na kuzungumza na wananchi wapendwa wa Jamhuri ya Kenya. Waliweza kunipatia malalamiko yao kuhusiana na maiti kuzuiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti."
}