GET /api/v0.1/hansard/entries/873840/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873840,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873840/?format=api",
    "text_counter": 123,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": "Sababu za vifo kwanza, tunasema kila nafsi itaonja mauti, kwa sababu ni Mwenyezi Mungu hupeana na pia ni yeye huchukua. Lakini kuna kuonja maiti kwa sababu ya udhalimu wa serikali iliyo mamlakani ambayo haitaki kuangalia maslahi ya mwananchi wa kawaida. Sababu ya kwanza inayosababisha vifo katika hospitali za umma humu nchini ni usimamizi mbovu wa visa vya maradhi. Kwa mfano, mwaka uliopita niliweza kuleta mjadala katika Bunge hili nikiitaka Serikali iweze kujenga hospitali moja ya rufaa katika kaunti zote 47 humu nchini."
}