GET /api/v0.1/hansard/entries/873852/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873852,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873852/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": " Asante, Naibu Spika. Unajua wakati tuna mjadala mzito kama huu, ambao unasimamia maswala ya maskini wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mwezangu asijaribu kuleta mchezo ndani ya kazi. Lakini nesi ni sawa tu. Ni kama kusema nurse kwa Kizungu. Kwa hivyo, tunasema nesi ama daktari. Sipingani na hilo, ila tu kwamba ni lugha hauelewi. Lakini asante sana. Nilikuwa nazungumia madaktari na kusema kwamba tuko na elefu 11 dhidi ya Wakenya milioni 45. Dawa ni sababu ingine ya kufanya watu wetu wazidi kuumia. Hospitali zetu hazina dawa. Wagonjwa huenda hospitalini, mtu anapiga foleni kuanzia asubuhi hadi jioni na hapati dawa. Kifo chake kinasababishwa na dawa hizo kutopatikana. Tunaona katika hospitali nyingi humu nchini, dawa zinazofaa kutolewa kwa maskini zinachukuliwa na watu kadhaa wanaenda kuuza badala ya kuhudumia wananchi wa Kenya. Uhaba wa damu ni jambo lingine ambalo linasababisha watu wengi kufariki. Fedha haziwekezwi katika Bodi ya Kitaifa ya Damu. Hatuwekezi pesa za kuhakikisha kwamba tunapata damu ya kutosha. Kwa mfano, huwezi kupata matibabu ya saratani kama huna damu ya kutosha katika mwili wako. Maskini anayekula mboga na mahindi ya kuchemsha pale mtaani ataitoa wapi damu hii iwapo Serikali haizingatii na kuhakikisha kwamba maabara yetu yamejaa damu ya kuwapatia watu hawa bila malipo iwapo dharura itatokea? Dharura inapotokea ya mashambulizi, ndipo sisi sote kwa kauli moja tunajifanya kuwa Wakenya, we are one, twendeni tutoe damu. Tutakuwa tukitoa damu wakati wa visa vya ujambazi ama wakati wa visa vya ugaidi ama tutakuwa tukitoa damu ya kuhakikisha kwamba nchi hii iko na damu wakati wowote matatizo yatakapotokea?"
}