GET /api/v0.1/hansard/entries/873853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873853,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873853/?format=api",
    "text_counter": 136,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": "Nambari ya nne ni udhalimu wa Serikali. Leo niko radhi kusema kwamba Serikali imefeli wananchi wa Jamhuri ya Kenya. Serikali haiwekezi katika mambo ya maana. Leo Serikali inatoa bajeti kubwa kwa NYS, lakini haiwezi kutoa bajeti kubwa kwa afya. Tukitoa bajeti kubwa kwa National Youth Service (NYS), inaporwa na watu. Hatutoi bajeti kwa afya kuhakikisha kwamba tumeboresha hospitali zetu au kuhakikisha tuna vifaa spesheli vya kupambana na maradhi aina mbalimbali. Leo katika Bunge hili, tuna Wabunge 13 ambao wana saratani. Inafaa ituume na kusema kwamba hata sisi ni wagonjwa. Kwa nini tusiwatetee wale wako nje kwa sababu tuna nguvu na sauti ya kupigania suala hilo? Kwa nini tusitunge sheria… The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}