GET /api/v0.1/hansard/entries/873857/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873857,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873857/?format=api",
"text_counter": 140,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, Independent",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Nakubaliana na kauli mbiu yako lakini inafaa ujue Serikali ni sisi na Serikali ni wananchi wa Jamhuri ya Kenya. Bila ya wananchi, sisi hatuwezi kukaa hapa. Lakini nimekubaliana na kauli mbiu yako na nasema asante sana. Nilikuwa nazungumzia udhalimu wa Serikali kwa kufeli kuwahudumia wananchi wa Kenya kiafya na kusema kwamba imekataa kuwekeza katika afya. Nataka pia kuzungumzia ugatuzi wa afya kwa sababu kule mashinani, tunapata shida sana. Hatuwezi sisi kama Wabunge kutatua masuala ya afya mashinani kwa sababu ya ugatuzi. Hii imeleta balaa. Kuna baadhi ya viongozi kutoka kaunti mbali mbali ambao, badala ya kuwafikia wananchi na kuwasaidia, imekuwa kwamba fedha za afya wanazitenga kando na kuzitumia katika mambo mengine. Migomo ya kila mara ni sababu nyingine ya vifo. Inatuletea matatizo hapa nchini Kenya. Huduma ya National Hospital Insurance Fund (NHIF) ni jambo lingine ningependa kuzungumzia. Ndio kuna NHIF, lakini maskini wa kawaida anaweza kulipa ada hii kila mwezi ili kuhahakisha kwamba wakati wa dharura ataweza kujimudu? National Hospital Insurance Fund ina kauli mbiu moja: chukua ama uache! Shida ni yako. Ni lazima tuangalie ni vipi tutafanyia mwananchi wa kawaida iwe ndogo kwake ili aweze kupata matibabu ya kiafya. Kuna Big Four Agenda ambayo tunaizungumzia. Mojawapo ndani ya Big Four Agenda ni afya na tumejipiga kifua na kusema kwamba katika kipindi kilichosalia cha miaka mitatu, tutahakikisha kwamba tumeweza kufaulu katika kusukuma gurudumu la Big Four na kuhakikisha kwamba mambo yamekuwa sawasawa. Kwanza kabisa, tukizungumza masuala ya Big Four, tunasema rejesheni huduma zote za afya kwa Serikali ya Kitaifa kwa mujibu wa Kipengele cha 187 cha Katiba ya Kenya. Ni kwa nini tunasema murejeshe huduma za afya kwa Serikali? Ni kwa sababu Serikali hapo awali ilipokuwa ikisimamia masuala ya afya, iliweza kuhakikisha kwamba mwananchi wa kawaida hateseki. Leo pesa zilizoko mikononi mwa magavana hazifikii watoto wa maskini. Leo pesa ziko mikononi mwa magavana na haziwezi kuwasaidia maskini. Zamani, Wabunge walikuwa na fedha na uwezo wa kujenga zahanati au kwa lugha ya kimombo dispensary . Tulikuwa tunaweza kuwajengea watu kule mashinani. Leo mikono yetu imefungwa na hatuwezi kuwajengea. Magavana wote nchini Kenya waliojaliwa kupewa pesa za afya hawasaidii. Ni wachache tu. Kwa mfano, tunaona Gavana wa Makueni amefanya kazi ya maana. Je, kwa nini magavana wengine wapewe pesa za wananchi iwapo hawawezi kujenga hospitali? Kama wameshindwa, na sisi tupewe tujaribu kuwahudumia wananchi ama iregeshwe katika Serikali ya Taifa. Pili, ongezeni hospitali za Level 5. Tuna hospitali 11 za Level 5 Kenya nzima. Ziongezeni na muzipandishe cheo ziwe hospitali za rufaa ili mwananchi wa kawaida aweze kufikia hospitali hizi na kupata matibabu spesheli katika hospitali hizo. Tatu, tunasema kuwe na tume ya afya. Kukiwa na tume ya afya, hatutakuwa na masuala ya madaktari bandia, masuala ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}