GET /api/v0.1/hansard/entries/873858/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873858,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873858/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, Independent",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": "usimamizi wa hospitali au masuala ya matatizo yanayotokea. Juzi katika runinga tuliona jamaa ameenda katika hospitali ya Kenyatta akaiba mtoto wake kwa sababu ameshindwa kulipa Sh56,000. Na waibe watoto wawapeleke nyumbani kama serikali inashindwa kuwaangalia. Kwa nini tunaona vituko kama hivi vinatokea? Tunaona mtu anaenda hospitalini sio mwizi wa kawaida bali mwizi ambaye amedhulumiwa na anataka mtoto wake. Ni mwizi ambaye amepewa bei ambayo haiwezi. Mfuko wake hauwezi na Serikali hata haina huruma na maskini huyo inachukua pesa yake kwa kifua na kama huna pesa inachukua mtoto wako kwa kifua. Hatuwezi kuzalisha shida kila siku kukicha katika Jamhuri hii ya Kenya. Tume ya afya isimamie usajili, uhamisho, mishahara na vyeo vya madaktari ili mambo yaweze kwenda sambamba. Pesa zitoke Wizara ya Fedha hadi kwenye hospitali. Haya mambo ya pesa kutoka Wizara ya Fedha na kupitia sehemu mbalimbali bila kufikia hospitali inakuwa changamoto nyingine. Kuwe na mikakati ya kisasa ya kuendesha hospitali za rufaa ili asilimia 80 ya maskini waweze kusaidiwa. Fedha za afya kwa kaunti zilindwe kabisa. Mhe. Naibu Spika, sasa nitakueleza. Labda hamjui kwa siku moja watu wanaokufa ni maskini wala si mabosi. Mabosi hufa kwa mpango kwa sababu wana nguvu ya kujitibu. Maskini wanakufa kila siku. Kwa mfano nitakupatia Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta peke yake. Mtu anapofariki, kwa maiti kukaa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Kenyatta, usiku mmoja maskini anatakiwa alipe Sh4,900. Hiyo ni Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, Hospitali ya Coast General Mombasa na Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Eldoret, ambazo ni hospitali za rufaa, ada kwa siku ni Sh4,900. Maskini hata pesa za kununua Panadol hana na leo mtoto wake amekufa kwa sababu ya udhalimu wa Serikali, kwa sababu vifaa haviko, kwa sababu dawa haziko na kwa sababu wodi zimejaaa watu wanalala chini, umemtesa katika wodi hiyo miaka yote na sasa unataka kumtesa akiwa maiti na kuitisha Sh4,900 kila siku. Maskini hana la kufanya ataenda kufanya harambee. Akienda harambee maiti itakaa zaidi ya siku 20. Bei yake inakuwa ghali mno kushinda bei aliyokuwa akiitishwa hospitalini. Je, atalipa hospitali, achukue maiti ama aende kufanya nini? Serikali haina huruma kwa watu wake. Alisema wakati mmoja, Mheshimiwa James Orengo, kwamba Serikali hula watoto wake. Wewe ni maiti na bado Serikali inakutamani. Usipochukua maiti, Serikali itatumia maiti hiyo kwa mafunzo. Watachukua maiti hiyo na waipeleke kwa watoto wasomi wanaojifunza na mwili wa mtoto wako utapasuliwa na ufanyiwe mafunzo ya upasuaji. Turuhusu masikini wazike watoto wao. Tuwakumbuke masikini. Kila wiki nikienda Mombasa, nina matanga kama 10 ama 15. Sina pesa za kuwapa. Sina pesa za wizi. Tunapata shida tukifanya hivyo. Itakuwa afueni kwa Wabunge wote. Wacheni maskini wazike watoto wao. Kila siku, miili 25 isiyojulikana inatupwa na kufanyiwa utafiti. Aidha inakatakatwa inatupwa ama inafanyiwa utafiti. Hii ni miili ambayo haijulikani. Mtu amefiwa na mtoto wake, mzee wake, babake, mamake ama dadake na anaishi kule Kainuk Turkana. Ameleta mtoto, mzee ama babake katika Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta akiamini kwamba atapata matibabu. Hana nauli ya kurudi Turkana. Anafika kule na kusema ameachia Mwenyezi Mungu kwa sababu hana la kufanya kwa sababu mwili umezuiliwa. Naona muda unazidi kunipa kisogo. Kila siku, watu 25 wanatupwa ; 25 hufariki kila siku. Je, ni nani atazungumzia wanyonge? Ni nani atawatetea wanyonge? Naomba Bunge hili lipitishe Hoja hii kwa kauli moja ili masikini azike mtoto wake. Mheshimiwa Naibu Spika, atakayeafiki Hoja hii siku ya leo ni Mbunge machachari, kijana kama mimi kutoka Embakasi West, Mheshimiwa George Theuri. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}