GET /api/v0.1/hansard/entries/873860/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873860,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873860/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Embakasi West, JP",
    "speaker_title": "Hon. George Theuri",
    "speaker": {
        "id": 1429,
        "legal_name": "George Theuri",
        "slug": "george-theuri"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Naunga mkono Hoja hii ya kufutilia mbali ada za matibabu katika hospitali za umma za rufaa pindi mtu anapofariki. Kwa kweli sisi sote kama Wabunge tunajua ile shida tunayo. Shida kubwa ni kwamba katika kila eneo, kuna masikini wengi ambao huwapeleka watoto wao ama wapendwa wao katika hospitali za umma. Shida huwa baada ya mtu kumpoteza mtoto wake au mpendwa wake, unakuta kwamba hospitali zinawaambia walipe ada ya hospitali. Kuna harambee nyingi sana. Wengi ambao huachwa nyuma huwa ni watu hawajiwezi na wanalazimishwa kulipa. Wanapolipa unapata kwamba familia haziwezi kujitegemea. Namuunga mkono mwenzangu Mohamed. Ni vizuri Serikali iangalie jinsi inavyoweza kugharamia hasa wale watu ambao wamepoteza watoto wao ama watu wao katika hospitali za umma. Wapewe wapendwa wao wawazike bila kutozwa hiyo ada ya hospitali."
}