GET /api/v0.1/hansard/entries/873868/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873868,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873868/?format=api",
    "text_counter": 151,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nandi CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Tecla Tum",
    "speaker": {
        "id": 913,
        "legal_name": "Tum Tecla Chebet",
        "slug": "tum-tecla-chebet"
    },
    "content": " Asante, Naibu Spika. Naunga mkono Hoja hii ya kufutilia mbali ada za matibabu katika hospitali za umma za rufaa pindi mtu anapofariki na anaposhindwa kulipa. Tulipopata Uhuru mwaka wa 1963, tulitaka kuangamiza ugonjwa, umasikini na ujinga. Lakini sasa, kutatua mambo hayo imekuwa vigumu. Magonjwa ya saratani na figo yanadhuru watu wetu sana. Wengi wanakufa na kukaa katika hospitali kwa miezi miwili ama mitatu kwa sababu familia zao hazina pesa za kulipa. Ujinga umezidi kwa sababu watu wanauza mashamba yao ili walipe ada za hospitali. Naunga mkono Hoja hii kwa sababu umasikini umezidi ; mashamba yanauzwa ; watoto wanabaki nyumbani na hawaendi shule kwa sababu kile wazazi walikuwa nacho kimeisha kwa kugharamia ada za hospitali. Watoto hawana nyumba. Naunga mkono Hoja hii ili tusilipe ada za hospitali mtu akifariki. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}