GET /api/v0.1/hansard/entries/873875/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873875,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873875/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Butere, ANC",
"speaker_title": "Hon. Nicholas Mwale",
"speaker": {
"id": 13311,
"legal_name": "Nicholas Scott Tindi Mwale",
"slug": "nicholas-scott-tindi-mwale"
},
"content": "Kabla Wakenya wengi hawajapelekwa katika hospitali ya rufaa, wengi huwa wameenda kwanza katika hospitali ndogo, wametibiwa hapo, halafu wanapewa barua ambazo zinawaeleza kwamba wanafaa waende katika hospitali za rufaa. Kabla Wakenya wengi hawajafika katika hospitali za rufaa, huwa wametumia pesa nyingi katika hospitali za chini. Wanapofika kwenye hospitali za rufaa na bahati mbaya mmoja wao anafariki, Serikali inataka jamii ya mfu walipe ada ya matibabu ya mwendazake kabla wachukue maiti. Umaskini katika nchi yetu ya Kenya uko juu zaidi. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii. Siyo ada ya matibabu ya mtu ambaye amefariki peke yake inayofaa kufutiliwa mbali. Kama mtu ametibiwa na amepona, asizuiliwe katika hospitali ndio alipe ada ya matibabu ili aruhusiwe kwenda nyumbani."
}