GET /api/v0.1/hansard/entries/873878/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873878,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873878/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Butere, ANC",
"speaker_title": "Hon. Nicholas Mwale",
"speaker": {
"id": 13311,
"legal_name": "Nicholas Scott Tindi Mwale",
"slug": "nicholas-scott-tindi-mwale"
},
"content": "Naunga mkono Hoja hii. Madaktari katika Kenya, pamoja na wale ambao Serikali ilitoa katika nchi ya Cuba, ni 11,000. Wakenya wote ni milioni 45. Ukipiga hesabu, utapata daktari mmoja Kenya, ukiongeza wale ambao walitolewa katika nchi ya Cuba, anatibu Wakenya 5,000. Hao ni watu wengi. Hali hiyo inawaumiza Wakenya zaidi. Naunga mkono Mbunge mwenzangu, Mhe. Mohamed Ali, kwa sababu Serikali inafaa kutenga fedha za kushughulikia jambo hili, hata kama wamesema ni sisi tunafanya hivyo ambao ni ukweli. Wakati tunaweka pesa katika Bajeti, tunafaa kuweka pesa ambazo zitawasaidia maskini na Mkenya wa kawaida kufaidika katika mambo ya bima ya afya na matibabu."
}